Machapisho

TUPINGE UKATAJI WA MABOMBA YA MOSHI KWENYE PIKIPIKI

Picha
𝙋𝙞𝙘𝙝𝙖: 𝙈𝙖𝙙𝙚𝙧𝙚𝙫𝙖 𝙬𝙖 𝙗𝙤𝙙𝙖𝙗𝙤𝙙𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙞𝙨𝙞𝙠𝙞𝙡𝙞𝙯𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙡𝙚𝙠𝙚𝙯𝙤 𝙠𝙪𝙩𝙤𝙠𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙖𝙨𝙠𝙖𝙧𝙞 𝙬𝙖 𝙪𝙨𝙖𝙡𝙖𝙢𝙖 𝙗𝙖𝙧𝙖𝙗𝙖𝙧𝙖𝙣𝙞 𝙠𝙪𝙝𝙪𝙨𝙪 𝙪𝙢𝙪𝙝𝙞𝙢𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙥𝙞𝙣𝙜𝙖 𝙠𝙚𝙡𝙚𝙡𝙚 𝙯𝙞𝙣𝙖𝙯𝙤𝙩𝙤𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙣𝙖 𝙢𝙖𝙗𝙤𝙢𝙗𝙖 𝙮𝙖 𝙢𝙤𝙨𝙝𝙞 𝙮𝙖𝙡𝙞𝙮𝙤𝙠𝙖𝙩𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙥𝙞𝙠𝙞𝙥𝙞𝙠𝙞. 𝙃𝙞𝙞 𝙣𝙞 𝙏𝙝𝙖𝙙𝙚𝙤 𝙈𝙚𝙙𝙞𝙖 𝗟𝗲𝗼 𝗠𝗮𝗿𝗰𝗵 𝟬𝟵, 𝟮𝟬𝟮𝟲 𝗠𝗮𝗱𝗲𝗿𝗲𝘃𝗮 𝘄𝗮 𝗽𝗶𝗸𝗶𝗽𝗶𝗸𝗶 𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗯𝗲𝗯𝗮 𝗮𝗯𝗶𝗿𝗶𝗮, 𝗺𝗮𝗮𝗿𝘂𝗳𝘂 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝗯𝗼𝗱𝗮𝗯𝗼𝗱𝗮, 𝗺𝗸𝗼𝗮𝗻𝗶 𝗦𝗵𝗶𝗻𝘆𝗮𝗻𝗴𝗮 𝘄𝗮𝗺𝗲𝗽𝗲𝘄𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗵𝗮𝗺𝗮𝘀𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗶𝗻𝗴𝗮 𝘃𝗶𝘁𝗲𝗻𝗱𝗼 𝘃𝘆𝗮 𝘂𝗵𝗮𝗿𝗶𝗯𝗶𝗳𝘂 𝗮𝘂 𝘂𝗸𝗮𝘁𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗯𝗼𝗺𝗯𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗼𝘀𝗵𝗶 (𝗲𝘅𝗵𝗮𝘂𝘀𝘁) 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗽𝗶𝗸𝗶𝗽𝗶𝗸𝗶. 𝗩𝗶𝘁𝗲𝗻𝗱𝗼 𝗵𝗶𝘃𝘆𝗼 𝗵𝘂𝘀𝗮𝗯𝗮𝗯𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗸𝗲𝗹𝗲𝗹𝗲 𝗻𝗮 𝗺𝗶𝗹𝗶𝗽𝘂𝗸𝗼 𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝘀𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗯𝗮𝗿𝗮𝗯𝗮𝗿𝗮𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗮𝗮 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶. 𝗔𝗸𝗶𝘁𝗼𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗵𝗶𝘆𝗼, 𝗔𝘀...

TRA SHINYANGA LIPA KODI KABLA YA MACHI 31

Picha
   Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bw. Emmanuel Maro  Machi 09, 2026 | Shinyanga Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority - TRA) Mkoa wa Shinyanga imewahimiza wafanyabiashara na wananchi kufanya makadirio ya kodi na kulipa kodi ya awamu ya kwanza kwa mwaka 2026 kabla au ifikapo tarehe 31 Machi 2026. Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bw. Emmanuel Maro, amesema kuwa ulipaji kodi kwa wakati ni wajibu wa kila raia na ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa. Ameeleza kuwa kodi inayolipwa kwa wakati inawezesha Serikali kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, shule, vituo vya afya, huduma za maji safi pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi. Aidha, Bw. Maro amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo, huku wanunuzi wakihimizwa kudai risiti hizo ili kulinda haki zao na kusaidia kuongeza uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa ...

TUACHE VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Picha
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga (TPF-Net) ambaye pia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, Machi 08, 2026 aliwaongoza Maafisa, Wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kata ya Uyogo, Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, ambapo pia yalihusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali. Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Mhita ameitaka jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, akisisitiza kuwa ukatili unadhoofisha ustawi wa familia na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Amehimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa za matukio ya ukatili ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika. Aidha, ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwaheshimu na kuwawezesha wanawake katika nyan...

UJUMBE WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUTOKA KWA RAIS WA KIMATAIFA

Picha
  Leo March 08, 2026 Rais wa Kimataifa wa Standup for Women Society (SWS), Deborah A. Ijadele-Adetona, ametoa wito kwa wanawake duniani kuendelea kushirikiana, kuinuana na kuwekeza kwa wenzao ili kuleta maendeleo ya jamii. Akitoa ujumbe wake International Women’s Day, amesema siku hiio ni fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kujenga familia, jamii na mataifa, pamoja na kuthamini jitihada za wale waliovunja vikwazo na kuendelea kupigania haki na maendeleo ya wanawake. Amesema kaulimbiu ya mwaka huu “Give to Gain” (Toa ili Upate) inasisitiza umuhimu wa kusaidiana, kufundishana na kuunda fursa kwa wanawake na wasichana ili kuimarisha maendeleo jumuishi katika jamii. Ameongeza kuwa SWS itaendelea kuhamasisha uwezeshaji wa wanawake, kukuza uongozi jumuishi unaozingatia usawa wa kijinsia na kujenga utamaduni wa mshikamano miongoni mwa wanawake duniani. Kwa ujumla, Katika ujumbe wake, amewahimiza wanawake kusimama imara katika malengo yao, kuamini katika uwezo wao na kuende...

MWANAMKE MSINGI WA MALEZI NA MAADILI KATIKA JAMII

Picha
Na Thadeo Media  Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Kahama, Martha Kapela, amesema mwanamke ndiye chanzo cha maadili katika jamii, huku akieleza kwamba yeye ndiye mlezi na msimamizi wa kwanza wa maadili nyumbani. Akizungumza leo Machi 7, 2026 katika kongamano la wanawake lilofanyika Manispaa ya Kahama, amesema kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, Kapela sema: "Kila jamii inategemea mwanamke kueneza maadili mema kwa familia na watoto, Hivyo wanawake tunawajibika kulinda maadili, hususan katika familia zetu kwani tuna nafasi muhimu katika kujenga jamii yenye tabia bora." Afisa huyo amebainisha kuwa maadhimisho ya siku hii yanatoa fursa kwa jamii kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika malezi, elimu ya maadili, na utunzaji wa familia hukub akiwahimiza waalimu kushirikiana katika malezi ya watoto shuleni. "Ni jukumu letu sote kuheshimu, kuthamini, na kuunga mkono jukumu la mwanamke katika malezi na maadili, Walimu pia mtusaidie...

POLISI DAR WAKAMATA WEVYE MILIO MIKALI YA PIKIPIKI NA MAGARI

Picha
  Picha hii ni ya mfano kwa madhumuni ya kuonesha tukio husika na sio tukio halisi lililotokea wakati wa kukamatwa kwa watuhumiwa. Chanzo: Thadeo Media Library Photo . Na, Thadeo Gelema  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha vyombo vya moto kwa kutoa milio mikali ya milipuko kinyume cha sheria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa Machi 06, 2026, watuhumiwa hao wanadaiwa kuendesha magari na pikipiki zenye kelele kali zinazofanana na milipuko, hali inayosababisha usumbufu na hofu kwa wananchi pamoja na kukiuka Sheria ya Usalama Barabarani. Watuhumiwa waliokamatwa ni Abdallah Masumbuko mkazi wa Tabata, Julius Dismas mkazi wa Mwananyamala, Salehe Ally mkazi wa Kijitonyama na Mohamed Rashid mkazi wa Magomeni. Wote wanashikiliwa na Polisi huku hatua zaidi za kisheria zikiendelea kuchukuliwa dhidi yao. Kwa ujumla, Jeshi la Polisi limewahimiza watumiaji wote wa barab...

TPF-NET: WANAWAKE 400 WANUFAIKA NA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA SHINYANGA

Picha
Hii ni Thadeo Media  Leo March 06, 2026 Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Fatuma Mtarimbo, ameongoza Maafisa Wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali kutoa elimu kwa jamii katika Kata ya Mondo, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kilele chake kitaadhimishwa tarehe 8 Machi 2026, huku maadhimisho ya kimkoa yakitarajiwa kufanyika katika Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga. Katika mpango huo, wanawake zaidi ya 400 wamenufaika na elimu iliyolenga kuongeza uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia, pamoja na kuhimiza jamii kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao za msingi ikiwemo haki ya kupata elimu. Aidha, Mkuu wa TPF-NET Wilaya ya Kahama, Mrakibu wa Polisi (SP) Flora Nangawe, amewahasa wazazi kuacha tabia ya kupakiza watoto wa shule kwa idadi kubwa kwenye vyombo vya usafiri, wakati mwingine zaidi ya watoto 10 k...