Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TRA SHINYANGA LIPA KODI KABLA YA MACHI 31

 


 Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bw. Emmanuel Maro 
Machi 09, 2026 | Shinyanga
Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority - TRA) Mkoa wa Shinyanga imewahimiza wafanyabiashara na wananchi kufanya makadirio ya kodi na kulipa kodi ya awamu ya kwanza kwa mwaka 2026 kabla au ifikapo tarehe 31 Machi 2026.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bw. Emmanuel Maro, amesema kuwa ulipaji kodi kwa wakati ni wajibu wa kila raia na ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa.

Ameeleza kuwa kodi inayolipwa kwa wakati inawezesha Serikali kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, shule, vituo vya afya, huduma za maji safi pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi.

Aidha, Bw. Maro amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo, huku wanunuzi wakihimizwa kudai risiti hizo ili kulinda haki zao na kusaidia kuongeza uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Kwa ujumla,Amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi katika kulipa kodi kwa wakati unachangia moja kwa moja maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀