UJUMBE WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUTOKA KWA RAIS WA KIMATAIFA
Leo March 08, 2026 Rais wa Kimataifa wa Standup for Women Society (SWS), Deborah A. Ijadele-Adetona, ametoa wito kwa wanawake duniani kuendelea kushirikiana, kuinuana na kuwekeza kwa wenzao ili kuleta maendeleo ya jamii.
Akitoa ujumbe wake International Women’s Day, amesema siku hiio ni fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kujenga familia, jamii na mataifa, pamoja na kuthamini jitihada za wale waliovunja vikwazo na kuendelea kupigania haki na maendeleo ya wanawake.
Amesema kaulimbiu ya mwaka huu “Give to Gain” (Toa ili Upate) inasisitiza umuhimu wa kusaidiana, kufundishana na kuunda fursa kwa wanawake na wasichana ili kuimarisha maendeleo jumuishi katika jamii.
Ameongeza kuwa SWS itaendelea kuhamasisha uwezeshaji wa wanawake, kukuza uongozi jumuishi unaozingatia usawa wa kijinsia na kujenga utamaduni wa mshikamano miongoni mwa wanawake duniani.
Kwa ujumla, Katika ujumbe wake, amewahimiza wanawake kusimama imara katika malengo yao, kuamini katika uwezo wao na kuendelea kuwainua wanawake wengine ili kujenga dunia yenye fursa sawa kwa kila mwanamke na msichana.
Maoni
Chapisha Maoni