TUACHE VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga (TPF-Net) ambaye pia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, Machi 08, 2026 aliwaongoza Maafisa, Wakaguzi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kata ya Uyogo, Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, ambapo pia yalihusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali. Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Mhita ameitaka jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, akisisitiza kuwa ukatili unadhoofisha ustawi wa familia na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Amehimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa za matukio ya ukatili ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Aidha, ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwaheshimu na kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo, akibainisha kuwa usawa na haki kwa wanawake ni msingi muhimu wa kujenga jamii yenye amani na maendeleo.





Kwa ujumla, jamii imetakiwa kushirikiana kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola, kuheshimu haki za kila mtu na kuimarisha mshikamano ili kujenga familia na jamii salama yenye maendeleo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀