Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2026

𝐉𝐄, 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀? 𝐋𝐈𝐌𝐀𝐎 𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐔 𝐊𝐈𝐔𝐍𝐆𝐎!

Picha
Na,Thadeo Gelema    Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa lishe na kilimo pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), limao limethibitishwa kuwa ni tunda (fruit) kutokana na kuwa na mbegu na kukua kutoka kwenye maua ya mmea. Taarifa hizo za kitaalamu zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu katika elimu ya lishe na kilimo, zikionyesha wazi kuwa limao ni sehemu ya matunda ya jamii ya machungwa (citrus fruits), ingawa katika matumizi ya jikoni hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha.

UBUNIFU NA UADILIFU UTEKELEZAJI MIRADI YA POLISI JAMII!

Picha
Na,Mwandishi wetu Shinyanga  Kamishna wa Polisi Jamii (CP) Alex Mkama amewataka askari wanaotekeleza majukumu ya Polisi Jamii kwenda sambamba na mabadiliko ya wakati kwa kutumia mbinu bunifu zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika jamii. CP Mkama ametoa wito huo wakati akizungumza na Polisi Kata kutoka wilaya za Kishapu na Shinyanga, Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na askari kutoka vikosi mbalimbali katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Manispaa ya Shinyanga. CP Mkama , amesisitiza umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya wananchi ili kuongeza ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika kudumisha amani na usalama. Aidha , amewahimiza askari hao kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya taaluma, uadilifu na uwajibikaji, huku akisisitiza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi. Vilevile , ameeleza kuwa ni mu...

𝐏𝐄𝐓𝐑𝐎𝐋𝐈 𝐘𝐀𝐒𝐇𝐔𝐊𝐀, 𝐃𝐈𝐙𝐄𝐋𝐈 𝐘𝐀𝐏𝐀𝐍𝐃𝐀

Picha
Na Mwandishi wetu  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika nchini kuanzia Juni 3, 2026. Katika mabadiliko hayo, bei ya petroli imepungua kwa Sh29 kwa lita, kutoka Sh4,115 hadi Sh4,086 kwa lita. Hata hivyo, bei ya dizeli imeongezeka kwa Sh85 kwa lita na sasa kuuzwa kwa Sh4,333 kutoka Sh4,248 ya mwezi Mei. EWURA imeeleza kuwa licha ya ongezeko hilo, Serikali imetoa ruzuku ya Sh534 kwa kila lita ya dizeli ili kupunguza athari kwa watumiaji na sekta mbalimbali za uchumi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Gerald Maganga, amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na hali ya machafuko na migogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, jambo lililosababisha kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia. Kwa ujumla , EWURA imezitaka kampuni zote za mafuta kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa na kuonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka maelekezo hayo. ​  

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 3,2026

Picha
Magazeti  

Breaking : UMMY MWALIMU MSHAURI WA RAIS SAMIA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bi. Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo umetangazwa leo Juni 2, 2026 kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Bi. Ummy Mwalimu ni mmoja wa viongozi wenye uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma nchini, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Serikali ya Tanzania. Katika kipindi cha uongozi wake, amewahi kuhudumu katika sekta za afya, mazingira, Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

ACHENI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Picha
Na, Mwandishi wetu Shinyanga  Maafisa usafirishaji katika Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuacha tabia ya kujichukulia Sheria mkononi pindi matukio ya ajali yanapotokea badala yake watoe taarifa Kituo Cha Polisi ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa. Akitoa elimu hiyo katika Stendi kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila ambapo amewataka Maafisa usafirishaji hao kuacha kushawishiana kufanya vitendo vinavyopelekea vurugu ikiwa ni pamoja kuchoma moto vyombo vya moto, kujeruhi mhusika kwenye ajali hiyo na kuharibu miundombinu Kwa kufanya hivyo ni kutoa hukumu isiyo halali na ni kinyume na Sheria za Nchi. Sajenti Ndimila amewaeleza madereva hao kuwa vitendo hivyo wakivifanya vinaweza kusababisha uharibifu, majeruhi au vifo kitu ambacho kinaweza kuwapelekea kuingia kwenye kesi ya jinai pia vitendo hivyo vinaweza kuwageukia wao pindi watakaposababisha ajali Kwa kipindi...