UBUNIFU NA UADILIFU UTEKELEZAJI MIRADI YA POLISI JAMII!

Na,Mwandishi wetu Shinyanga 

Kamishna wa Polisi Jamii (CP) Alex Mkama amewataka askari wanaotekeleza majukumu ya Polisi Jamii kwenda sambamba na mabadiliko ya wakati kwa kutumia mbinu bunifu zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika jamii.

CP Mkama ametoa wito huo wakati akizungumza na Polisi Kata kutoka wilaya za Kishapu na Shinyanga, Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na askari kutoka vikosi mbalimbali katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Manispaa ya Shinyanga.

CP Mkama, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya wananchi ili kuongeza ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika kudumisha amani na usalama.

Aidha, amewahimiza askari hao kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya taaluma, uadilifu na uwajibikaji, huku akisisitiza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi.

Vilevile, ameeleza kuwa ni muhimu kwa askari kutambua vihatarishi vinavyoweza kuathiri usalama wa jamii mapema, ikiwemo migogoro ya kijamii, ukatili wa kijinsia, uhalifu wa watoto pamoja na matishio mengine ya kiusalama, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati

Picha: Alex Mkama akizungumza na askari wa Polisi Kata, Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na askari kutoka vikosi mbalimbali mkoani Shinyanga, akisisitiza ubunifu, uadilifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii kwa lengo la kuimarisha usalama na ushirikiano na wananchi. 





kwa ujumla, CP Alex Mkama amewahimiza askari kuzingatia ubunifu, uadilifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii ili kuimarisha usalama, kujenga imani kwa wananchi na kudumisha amani katika jamii. .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐉𝐄, 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀? 𝐋𝐈𝐌𝐀𝐎 𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐔 𝐊𝐈𝐔𝐍𝐆𝐎!

𝐆𝐀𝐌𝐎𝐍𝐃𝐈; 𝐀𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀𝐙𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐒𝐓𝐀𝐑𝐒