𝐉𝐄, 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀? 𝐋𝐈𝐌𝐀𝐎 𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐔 𝐊𝐈𝐔𝐍𝐆𝐎!
Na,Thadeo Gelema Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa lishe na kilimo pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), limao limethibitishwa kuwa ni tunda (fruit) kutokana na kuwa na mbegu na kukua kutoka kwenye maua ya mmea. Taarifa hizo za kitaalamu zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu katika elimu ya lishe na kilimo, zikionyesha wazi kuwa limao ni sehemu ya matunda ya jamii ya machungwa (citrus fruits), ingawa katika matumizi ya jikoni hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha.

Maoni
Chapisha Maoni