Machapisho

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 02, 2026

Picha
Magazetini leo

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: 𝐒𝐄𝐋𝐄𝐂𝐓𝐈𝐎𝐍 𝐊𝐈𝐃𝐀𝐓𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐕𝐘𝐔𝐎 𝐕𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈 2026

Picha
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetangaza rasmi uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano pamoja na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2026 . 👉 BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI 

𝐌𝐈𝐆𝐎𝐆𝐎𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐈𝐃𝐈 𝐘𝐀 49,000 2025/26

Picha
Na Mwandishi Wetu mbungeni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema wizara hiyo ilipokea jumla ya mashauri 49,573 ya ndoa katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026. Akizungumza leo Juni 1, 2026 Bungeni, Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya mapitio ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2025/2026 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027, Dkt. Gwajima amesema: “Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, Wizara kwa kushirikiana na OWM–TAMISEMI ilipokea mashauri 49,573 ya ndoa.” Pia Waziri Gwajima amefafanua kuwa kati ya mashauri hayo, 9,995 yalisuluhishwa na kufungwa na 8,036 yalipelekwa Mahakamani, huku 31,542 yakiendelea kusuluhishwa. Kwa ujumla, Takwimu hizi zinaweza kuonesha picha ya jamii inayokabiliwa na mabadiliko ya kijamii, ambapo migogoro ya ndoa inaongezeka kutokana na sababu mbalimbali kama uchumi, mawasiliano duni na changamoto za malezi .

MOTO WATEKETEZA STUDIO ZA BARNABA CLASSIC

Picha
Na, mwandishi wetu Dar es Salaam  Studio za mwanamuziki wa Tanzania, Elias Barnabas maarufu kama Barnaba Classic, zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Juni 1, 2026 katika eneo la Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barnaba amesema moto huo ulianza majira ya saa 2:30 usiku muda mfupi baada ya kutoka kwenye shughuli zake za kikazi. Amesema studio hizo zilikuwa zimefanyiwa ukarabati mkubwa wiki chache zilizopita kwa gharama kubwa. Barnaba ameeleza kuwa tukio hilo limemuumiza kwa kuwa studio hizo zilikuwa zikitoa ajira na fursa kwa vijana wengi kupitia shughuli za muziki na uzalishaji wa kazi za sanaa. Kwa ujumla, Pamoja na hasara iliyotokea, msanii huyo amesema anamshukuru Mungu kwa uhai na kuahidi kuanza upya huku akichukulia tukio hilo kama funzo la maisha .

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 01,2026

Picha
Magazeti