𝐌𝐈𝐆𝐎𝐆𝐎𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐈𝐃𝐈 𝐘𝐀 49,000 2025/26


Na Mwandishi Wetu mbungeni

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema wizara hiyo ilipokea jumla ya mashauri 49,573 ya ndoa katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026.

Akizungumza leo Juni 1, 2026 Bungeni, Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya mapitio ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2025/2026 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027, Dkt. Gwajima amesema:

“Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, Wizara kwa kushirikiana na OWM–TAMISEMI ilipokea mashauri 49,573 ya ndoa.”

Pia Waziri Gwajima amefafanua kuwa kati ya mashauri hayo, 9,995 yalisuluhishwa na kufungwa na 8,036 yalipelekwa Mahakamani, huku 31,542 yakiendelea kusuluhishwa.

Kwa ujumla, Takwimu hizi zinaweza kuonesha picha ya jamii inayokabiliwa na mabadiliko ya kijamii, ambapo migogoro ya ndoa inaongezeka kutokana na sababu mbalimbali kama uchumi, mawasiliano duni na changamoto za malezi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐉𝐄, 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀? 𝐋𝐈𝐌𝐀𝐎 𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐔 𝐊𝐈𝐔𝐍𝐆𝐎!

𝐆𝐀𝐌𝐎𝐍𝐃𝐈; 𝐀𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀𝐙𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐒𝐓𝐀𝐑𝐒