MOTO WATEKETEZA STUDIO ZA BARNABA CLASSIC

Na, mwandishi wetu Dar es Salaam 

Studio za mwanamuziki wa Tanzania, Elias Barnabas maarufu kama Barnaba Classic, zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Juni 1, 2026 katika eneo la Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barnaba amesema moto huo ulianza majira ya saa 2:30 usiku muda mfupi baada ya kutoka kwenye shughuli zake za kikazi. Amesema studio hizo zilikuwa zimefanyiwa ukarabati mkubwa wiki chache zilizopita kwa gharama kubwa.

Barnaba ameeleza kuwa tukio hilo limemuumiza kwa kuwa studio hizo zilikuwa zikitoa ajira na fursa kwa vijana wengi kupitia shughuli za muziki na uzalishaji wa kazi za sanaa.

Kwa ujumla, Pamoja na hasara iliyotokea, msanii huyo amesema anamshukuru Mungu kwa uhai na kuahidi kuanza upya huku akichukulia tukio hilo kama funzo la maisha.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐉𝐄, 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀? 𝐋𝐈𝐌𝐀𝐎 𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐔 𝐊𝐈𝐔𝐍𝐆𝐎!

𝐆𝐀𝐌𝐎𝐍𝐃𝐈; 𝐀𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀𝐙𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐒𝐓𝐀𝐑𝐒