𝐊𝐈𝐒𝐀 𝐍𝐘𝐄𝐓𝐈: 𝐊𝐀𝐌𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀𝐏𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐑𝐄𝐉𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈

Na, Thadeo Gelema

Leo Aprili 14, 2026 Kamati ya Maridhiano mkoani Shinyanga imelipongeza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa juhudi zake za kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao, hususan katika kipindi hiki ambacho kumeibuka uvumi unaosababisha taharuki miongoni mwa wananchi ukidai kuwa mtu akiguswa begani hupoteza sehemu zake za siri kwa wanaume.

Picha: Viongozi wa Kamati ya Maridhiano mkoani Shinyanga wakiwa katika kikao cha majadiliano, wakijadili masuala ya kuimarisha amani, mshikamano na utulivu

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano,amani, mila na desturi mkoani humo, Shekhe Balilusa Khamis, akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, akiwa ameambatana na viongozi wengine wa dini mbalimbali, Mkuu wa Machifu pamoja na Kamanda wa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi. Amesema kuwa juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hofu kwa wananchi na kurejesha hali ya utulivu katika jamii.

Picha: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano, Shekhe Balilusa Khamis, akizungumza kuhusu hali ya amani mkoani Shinyanga.

Aidha,

 Shekhe Khamis ametoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa zisizo na ukweli na badala yake kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wa jamii. 

Picha: Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Maridhiano mkoani Shinyanga wakifuatilia kwa makini mjadala unaoendelea, wakionesha umakini na uzingativu katika kujadili masuala ya kuimarisha amani na utulivu wa jamii.

Ameongeza kuwa umoja na mshikamano wa viongozi wa dini na kimila ni nguzo muhimu katika kudumisha amani na utulivu.

Kwa upande wake, Mtemi Kidola wa II ambaye ni Mwenyekiti wa Machifu mkoani Shinyanga, amempongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo pamoja na wasaidizi wake kwa hatua wanazochukua dhidi ya watu wanaosambaza uvumi huo. 

Picha: Mtemi Kidola wa II akitoa pongezi kwa Polisi kwa hatua za haraka za kukomesha upotoshaji na kurejesha utulivu

Amesema kuwa kuwafikisha mahakamani wanaozusha taarifa hizo ni njia sahihi ya kukomesha upotoshaji unaoweza kusababisha taharuki na vurugu zisizo za lazima.

Kwa ujumla, Kamati hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola pamoja na wadau wengine katika kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili kuondoa hofu isiyo na msingi na kuimarisha mshikamano wa kijamii mkoani Shinyanga.


📲 Kwa habari zaidi, endelea kufuatilia Thadeo Media

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀