π¨πππππ¨ππ πͺπ π ππ₯π¨πππ’: π¦πππ₯π’π‘ ππ©π¨π‘ππ π¨ππ¨π§π π¦π§ππ’π¦π’
π 10 Aprili 2026
Shinyanga – Hatimaye pazia limefungwa katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, huku Sharon Callist Mathias akiandika historia kwa kuibuka mshindi na kuwa Rais mpya wa wanafunzi.
Uchaguzi huo uliokuwa umejaa presha, mvutano na matarajio makubwa, umegeuka kuwa gumzo kubwa chuoni hapo baada ya kuleta matokeo tofauti kabisa na uchaguzi wa awali.
MATOKEO RASMI YA MARUDIO
Sharon (Shaloni) — kura 23
Vicent — kura 11
Moris Daudi — kura 8
Maduhu — kura 5
Sitta — kura 2
Jumla ya kura: 49
Hakuna kura iliyoharibika
ILIVYOKUWA MWANZO
Katika uchaguzi wa kwanza, hali ilikuwa tofauti kabisa ambapo Maduhu aliongoza kwa kura 43, akifuatiwa na Sharon aliyepata kura 21. Hata hivyo, malalamiko juu ya mwenendo wa uchaguzi yalizua sintofahamu na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi.
MABADILIKO MAKUBWA
Uchaguzi wa marudio umeonyesha mabadiliko ya wazi ya maamuzi ya wapiga kura, ambapo Shaloni ameweza kupindua upepo na kuibuka mshindi, huku waliokuwa vinara awali wakishuka kwa kiasi kikubwa cha kura.
SHALONI NI NANI?
Aliwahi kuwa Makamu wa Rais STJOSO
Ni Katibu wa Hamasa UVCCM Mkoa wa Shinyanga
Sasa ni Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya STJOSO
Ushindi wake unaonekana kama ishara ya:
✔ Mabadiliko ya uongozi
✔ Kuimarika kwa nafasi ya wanawake
✔ Imani mpya kutoka kwa wanafunzi
WAPINZANI WAKUBWA
Vicent – Nafasi ya pili kwa kura 11
Moris Daudi – Kura 8
Maduhu – Alishuka hadi kura 5 licha ya kuongoza awali
Sitta – Kura 2
Kwa ujumla, Uchaguzi huu wa marudio umeacha ujumbe mmoja mkubwa:
π Nguvu ya kura inaweza kubadilisha kila kitu
Kutoka kuwa miongoni mwa wagombea hadi kuwa Rais, Shaloni ameonesha kuwa siasa za wanafunzi zinaweza kubadilika kwa muda mfupi sana.
π² Kwa habari zaidi, endelea kufuatilia Thadeo Media

Mkadumishe Mshikamano, Nidhamu, utendaji bora na kushilikiana bila ya chuki kwani uongozi ni service oriented is not only sitting on the throne but serving others Equallyπ
JibuFuta