𝗞𝗜𝗦𝗔 𝗡𝗬𝗘𝗧𝗜 𝗪𝗔𝗛𝗨𝗞𝗨𝗠𝗜𝗪𝗔 𝗝𝗘𝗟𝗔 𝗦𝗛𝗜𝗡𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kusambaza taarifa zisizo za kweli wakidai kuwepo kwa siri iliyopotea kimujiza baada ya kuguswa na benga, hali iliyozua hofu na taharuki kwa wananchi.
Ameeleza kuwa baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama, wawili hao walipatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo.
Katika hukumu iliyotolewa, Kisaka Elininhaki amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, huku Makoye James akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakumbusha wananchi kuwa kusambaza taarifa za uongo ni kosa la jinai na linaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.
Aidha, wananchi wametakiwa kutoa taarifa sahihi na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha amani na utulivu.
Kwa ujumla, Hukumu hii ni somo kwa jamii kuwa kusambaza taarifa za uongo kuna madhara makubwa na kunaweza kusababisha taharuki isiyo ya lazima. Ni muhimu wananchi kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza na kushirikiana na vyombo vya usalama ili kulinda amani na utulivu wa jamii.






Maoni
Chapisha Maoni