𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗪𝗔 𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢: 𝗝𝗘, 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗗𝗜𝗢 𝗙𝗨𝗥𝗦𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗞𝗜 𝗔𝗨?

 


Na, Thadeo Gelema 

📅 08 April 2026 | ⏰ Saa 15:20 Alasiri 


Shinyanga – Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) limehitimishwa rasmi, lakini hadi sasa hali ya sintofahamu imeendelea kutawala baada ya matokeo kuchelewa kutangazwa.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, zoezi la kupiga kura lilikamilika majira ya saa sita, huku kura zikihifadhiwa ndani ya chumba cha Dean of student, zikisubiri hatua zinazofuata katika mchakato wa kuhesabu na kutangaza matokeo.


Hadi sasa, baadhi ya wagombea pamoja na wafuasi wao bado wapo eneo la tukio wakisubiri, huku wakitarajia uwepo wa Mkurugenzi wa chuo ili kuendelea na hatua inayofuata. Wakati huo huo, baadhi ya wanafunzi wameanza kuondoka kutokana na kuchelewa kwa mchakato huo.


Hali hii imeendelea kuibua maswali miongoni mwa wanafunzi kuhusu uwazi na ufanisi wa usimamizi wa uchaguzi huo wa marudio, ambao tayari umebeba matarajio makubwa ya kurejesha imani ya wanafunzi.


Kwa ujumla, Wakati macho yote yakielekezwa kwa uongozi wa chuo, wanafunzi wanaendelea kusubiri kwa hamu kuona hatua zitakazochukuliwa, na kama kweli uchaguzi huu utakuwa mwanzo wa haki au chanzo cha mvutano mpya.

📲 Kwa habari zaidi, endelea kufuatilia Thadeo Media

Maoni

  1. Kwan kura huwa zina lala maana mhb mpk saiv hayjtok kulkoni

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀