CHUKUENI TAHADHARI MNAPOKIMBIA MCHAKAMCHAKA BARABARANI
| picha: Askari Polisi Koplo Zuhura Mlungwana akiwapa maelekezo ya usalama. |
Hii ni Thadeo Media
Leo Jumatano ya Februari 18, 2026 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyashimbi iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani Kwa kuchukua tahadhari pindi wawapo katika mazoezi ya mchakachaka barabarani.
Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Kahama Koplo Zuhura Mlungwana amewaelimisha wanafunzi hao kujipanga upande wa kushoto wa barabara ikiwa ndio upande sahihi wa kukimbilia wakiwa katika mazoezi yao pamoja na kuwapanga washika vibendera mbele ya kundi na nyuma ili waweze kuongoza kundi hilo barabarani
Koplo Zuhura amewasisitiza kujipanga mistari mitatu hadi minne wakati wa mazoezi ili kupunguza msongamano barabarani na kuepuka ajali pindi watakapo kanyagana na kuanguka.
Picha: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyashimbi wakiwa kwenye mazoezi ya mchakachaka barabarani, wakiwa wamepangwa vizuri huku polisi akiwapa maelekezo ya usalama.
Kwa ujumla, Elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Nyashimbi ni muhimu ili kuzuia ajali. Wanafunzi wanashauriwa kuzingatia mafunzo ya polisi na kushirikiana kuhakikisha mazoezi ya mchakachaka yanafanyika salama.
Kwel
JibuFuta