MWENYEKITI UMIKIDO AKUTANA NA WAZIRI KATAMBI KUJADILI MAADILI YA HABARI MTANDAONI

 Hii ni Thadeo Media 


Dodoma.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, leo Januari 28, 2026 Majata alimweleza Waziri Katambi juu ya malengo ya UMIKIDO katika kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali.

Waziri Katambi amepongeza hatua ya umoja huo kujitambulisha, na ameuhimiza UMIKIDO kufika ofisini kwake ili kufanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimaadili, matumizi salama ya mitandao, pamoja na namna vyombo vya habari mtandaoni vinavyoweza kushirikiana na serikali katika kulinda usalama na maslahi ya Taifa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀