Habari

Kesi ya Jengo la Ghorofa Kariakoo: Wawili Waachiwa Huru, Hatima ya WashtakiwaWanne Yabaki Kitendawili

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washtakiwa wawili kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa, eneo la Kariakoo.

Wawili hao ambao ni Zenabu Silam (61) na Ashour Awadhi Ashour (38) wameachiwa huru leo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kusema hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Olembelle kumueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ya kwamba DPP amewasilisha hati ya kutoendelea na kesi dhidi ya washtakiwa hao wawili.

Washtakiwa wanne waliobaki katika kesi hiyo ni Leondela Mdete (49), Soster Nziku (55), Aloyce Sangawe (59) na Stephen Nziku (28) wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Washtakiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo, Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Congo eneo la Kariakoo ambapo isivyo halali walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya watu 31.

Uamuzi wa Mahakama kuachia huru wawili katika kesi ya jengo la ghorofa Kariakoo unatoa taswira ya haki kisheria, huku washtakiwa wanne waliobaki wakikabiliwa na kesi nzito. Tukio hili linafunua changamoto za uwajibikaji wa majengo, usalama wa wananchi, na umuhimu wa mfumo wa kisheria kuhakikisha haki inatendeka kwa wote bila upendeleo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀