Habari
Dkt. Mwinyi Aongoza Baraza la Mapinduzi na Kuapisha Mkuu wa Mkoa
Na Thadeo Media
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao cha Kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) cha Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Disemba 2025, Ikulu, Zanzibar.
Kikao hicho cha BLM pia kimeambatana na uapisho, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyemteua hivi karibuni.
Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mgeni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba.
Kikao hiki kinaashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali ya Awamu ya Nane katika Kipindi cha Pili, kikionesha dhamira ya kuimarisha utawala bora na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.
Maoni
Chapisha Maoni