Michezo
Vilabu vinne vya Tanzania Kesho Kuanza Safari ya Kimataifa CAF
Na Thadeo Gelema
Septemba 18, 2025
Vilabu vinne vikubwa vya Tanzania – Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Singida Black Stars – vipo tayari kwa mapambano ya kimataifa katika michuano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup wikiendi hii, ambapo mchezo wa kwanza utaanza kesho Ijumaa, Septemba 19, 2025.
Yanga SC vs Wiliete SC (Angola)
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wataanza safari yao kwa kuvaana na Wiliete SC ya Angola kesho Ijumaa, Septemba 19, saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa EstΓ‘dio 11 de Novembro huko Benguela.
Marudiano yatapigwa Dar es Salaam, Septemba 26, 2025.
Katika michuano ya CAF Confederation Cup, Azam FC nao wataanza kesho Ijumaa, Septemba 19, saa 12:00 jioni, dhidi ya El Merrikh SC ya Sudan kwenye Uwanja wa Juba National Stadium, Sudan Kusini.
Marudiano yatafanyika Dar es Salaam, Septemba 26, 2025.
Singida Black Stars vs Rayon Sports (Rwanda)
Singida Black Stars watafungua dimba lao kwa kusafiri hadi Kigali, Rwanda kucheza na Rayon Sports kesho Ijumaa, Septemba 19, saa 9:00 usiku kwenye Nyamirambo Stadium.
Marudiano yatapigwa Singida, Septemba 26, 2025.
Simba SC vs Gaborone United (Botswana)
Wawakilishi wengine kwenye Champions League, Simba SC, wao wataingia dimbani Jumamosi, Septemba 20, saa 12:00 jioni dhidi ya Gaborone United kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume Stadium mjini Francistown, Botswana.
Marudiano yatafanyika Dar es Salaam, Septemba 27, 2025.
Hatua ya Mashindano
Michezo hii ni ya mzunguko wa awali ambapo washindi kwa jumla ya mechi mbili wataendelea hatua inayofuata ya michuano ya CAF. Mashabiki wa soka nchini Tanzania wamesema matarajio yao ni kuona vilabu vyote vikipeperusha vyema bendera ya taifa, huku safari ikianza kesho rasm
Maoni
Chapisha Maoni