Maisha ya chuoni
Picha Semina ya Kujenga Kiongozi Bora Yafungwa Rasmi St. Joseph Shinyanga, Wanafunzi Watatu Wavuna Vyeti
Shinyanga, Agosti 29, 2025 – Semina ya siku tatu ya Ujasiriamali na Akili Timamu (Emotional Intelligence) imehitimishwa leo katika Chuo cha Mtakatifu Joseph Shinyanga kwa washiriki watatu kupokea vyeti rasmi vya umahiri baada ya kufaulu mitihani ya mafunzo.
Walioibuka kidedea ni:
1. Elisha Joseph
2. Yusuph Abdi – Kaimu wa Rais wa Chuo
3. Devotha Charles
Wanafunzi hao walipongezwa kwa kuonyesha uelewa wa kina katika masuala ya uongozi, ujasiriamali na matumizi ya akili timamu katika maisha ya kila siku.
Kuhusu Semina
Semina hii ilianza rasmi Agosti 27, 2025 kwa ushirikiano na JA Afrika, ikilenga kuwajengea wanafunzi msingi wa kuwa viongozi bora na wabunifu wa kijasiriamali.
Katika mafunzo hayo, washiriki walijifunza nguzo kuu za Emotional Intelligence zikiwemo:
Kujitambua (Self-Awareness)
Kujidhibiti (Self-Management)
Huruma (Empathy)
Uongozi wa Kijamii (Social Intelligence)
Aidha, wageni kutoka JA Afrika walisisitiza sifa kuu za kiongozi bora kama vile kujiamini, uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha, kutatua matatizo kwa ubunifu, kujenga utamaduni chanya, na kudumisha uhusiano mzuri na watu.
Washiriki Walivyopokea Mafunzo
Wanafunzi walimshukuru Mwalimu muelimishaji kutoka JA Afrika pamoja na wageni waalikwa kwa kuwapa nafasi hiyo ya kipekee. Walisema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya mabadiliko kwa maisha yao ya kielimu, kijamii na hata katika uongozi wao wa kila siku chuoni.
Shukrani na Hitimisho
Akifunga rasmi semina hii, mlezi wa wanafunzi aliwapongeza washiriki wote na kuwataka kuyatumia mafunzo hayo kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Aidha, alisisitiza kuwa vyeti vilivyotolewa ni alama ya kutambua juhudi na kujituma kwa washiriki waliofanya vizuri zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni