Maisha ya chuoni

 PICHA: MAPUMZIKO YA MTIHANI – WANAFUNZI WAKIJIANDAA NA MTIHANI WA MCHANA ST. JOSEPH’S COLLEGE



 St. Joseph’s College – Shinyanga

Jumatatu, 28 Julai 2025

Siku ya kwanza ya mitihani ya mwezi Julai chuoni St. Joseph’s College Shinyanga imeanza rasmi leo asubuhi kuanzia saa 2:00. Baada ya mtihani wa awali, wanafunzi walipata mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mtihani wa mchana unaoanza saa 6:00.

Katika muda huo wa mapumziko, wanafunzi wameonekana wakijisomea, kujadiliana na kutafakari mada mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mtihani wa mchana. Sehemu mbalimbali za chuo zilijaa utulivu huku mazingira yakibeba hali ya kujiandaa kwa bidii na umakini hasa.

Mitihani hii imepangwa kuendelea hadi Ijumaa, Agosti 1, 2025, kwa ratiba maalum iliyotolewa mapema wiki iliyopita.

Wanafunzi wakipumzika kwa muda mfupi wakisubiri mtihani wa saa 6:00 mchana



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀