Maisha ya chuoni
ST. JOSEPH’S – WIKI YA KUJIPAMBANUA KIUWEZO YAWASILI: BAADA YA WANAFUNZI KUKABIDHIWA NAMBA, VYUMBA KUPANGWA, MITIHANI KUANZA KESHO – JULAI 28
jumapili, 27 Julai 2025
Thadeo Media
Wiki ya mwisho kabla ya kuanza rasmi kwa mitihani ya muhula imehitimishwa leo kwa pilikapilika nyingi na maandalizi makubwa, yakiwamo ugawaji wa namba rasmi za mtihani na upangaji wa vyumba kwa uangalifu mkubwa. Hali hii inaonyesha wazi kuwa wiki ya kujipambanua kiu uamuzi kielimu imetimia.
NAMBA ZA MITIHANI ZILIGAWIWA KWA UMAKINI KWA UJUMULA
Katika mfululizo wa maandalizi yaliyodumu kwa wiki nzima, wanafunzi walipokea namba za mitihani kwa awamu na kwa makundi tofauti kulingana na ratiba na utekelezaji wa masharti. Ugawaji huu ulizingatia kwa karibu masharti muhimu ikiwemo malipo ya ada, kukamilisha coursework, na kufikia alama zinazokubalika kwenye test za ndani.
Mchakato mzima uliwekwa chini ya usimamizi wa idara ya mitihani na menejimenti ya chuo, kuhakikisha kila mwanafunzi anapata nambari yake rasmi kwa utaratibu bila mchanganyiko wowote.
NAMBA ZA MITIHANI ZILITOLEWA RASMI – KWAMASHARTI.
Wanafunzi walipewa namba baada ya kuthibitisha kutimiza masharti yafuatayo:
Kulipa ada zote za muhula bila deni,
Kuwasilisha na kusaini coursework na assessments zote muhimu,
Kupata alama ya kupitisha kwenye test za ndani (Continuous Assessment), ambapo wanafunzi waliopata chini ya alama husika hawaruhusiwi kuchukua namba hata hivyo hazipo taarifa za mwanafunzi kutotimiza sharti hili
Kujiandikisha rasmi na kusaini orodha ya wanafunzi wa kozi husika,
Kuwa na nidhamu bora isiyokiuka kanuni za chuo.
VYUMBA VYA MITIHANI VIMEPANGWA KWA UMAKINI MKUBWA
ya chuo Hasa uongozi wa (STJOSO) imehakikisha vyumba vyote vya mitihani vimepangiliwa kwa kuzingatia idadi ya wanafunzi na taratibu za kitaaluma. ili kuepusha mkanganyiko siku ya mtihani.
Kwa sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka wizara au mamlaka za juu kuhusu mabadiliko yoyote ya ratiba, hivyo mitihani inaendelea kama ilivyopangwa kuanzia kesho, Julai 28.
Wiki hii ya mwisho kabla ya mtihani imejaa harakati nyingi: wanafunzi walijitahidi kukamilisha kazi zao, walipokea namba za mtihani, wakapanga ratiba zao za kusoma, na vyumba vikiwa tayari kwa mpangilio madhubuti.
Kwa maneno ya methali ya Kiswahili:
“Mtaka cha uvunguni sharti ainame.”
Hii imekuwa wiki ya jitihada kubwa, shinikizo, na kujiandaa kwa dhati kwa ajili ya mtihani wa mwisho unaoanza kesho
UJUMBE WA THADEO MEDIA
Mitihani si adhabu bali ni fursa ya kuonesha juhudi zako zote. Kwa kila mwanafunzi wa St. Joseph’s College – Shinyanga, tunawatakia mafanikio mema na mtaalamu wa kuendeleza masomo na ndoto zenu.
Endelea kufuatilia Thadeo Media kwa taarifa na picha za kweli kutoka chuoni.
Maoni
Chapisha Maoni