Maisha ya chuoni
ZIARA YA MAADILI YA KIUTU ILIFANA ST. JOSEPH'S COLLEGE – WAHITIMU WALIJIFUNZA KWA VITENDO KUGUSA MAISHA.
Bushushu – Shinyanga Society Offers
Taarifa rasmi: Jumapili, 27 Julai 2025
Katika kuendeleza maadili ya utu, huruma na mshikamano wa kijamii, wanafunzi wa St. Joseph’s College – Shinyanga wamehitimisha kwa mafanikio ziara ya kipekee ya kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha Shinyanga Society Offers – Bushushu.
Ziara hiyo iliyofanyika jana, Jumamosi, Julai 26, iliwakutanisha wanafunzi, viongozi wa serikali ya wanafunzi na walimu walezi katika safari ya kiroho yenye kugusa mioyo na kubadili mitazamo. Wakiwa kituoni, wanafunzi walishiriki shughuli mbalimbali ikiwemo:
SHUGHULI WALIZOFANYA:
Kukabidhi misaada ya kijamii (sabuni, vifaa vya shule, na fedha)
Kuzungumza na watoto na walezi wao
Kujifunza changamoto za maisha ya wenye mahitaji maalum
Kutoa neno la faraja, upendo na tumaini kama
“Kuwahudumia waliopuuzwa si ukarimu wa muda mfupi, bali ni wajibu wa kila mmoja wetu.”
MISAADA ILIYOKABIDHIWA:
Sabuni na vifaa vya usafi,Kalamu na daftari, Fedha taslimu – kwa matumizi ya dharura ya kituo
Misaada hiyo ilikusanywa kwa moyo wa hiari na mshikamano miongoni mwa wanafunzi, walimu na wadau wa chuo.
TUKIO KWA PICHA:
Picha mbalimbali zilizoambatana na ziara hiyo zinaonesha wanafunzi wakiwa bega kwa bega na watoto wa kituoni, kuzungumuza nao.
KAULIMBIU YA ZIARA:
"Tunapowajali waliopuuzwa, ndipo tunapofikia maana halisi ya utu."
UJUMBE KWA WANAJUMUIYA KUTOKA KWA WAZIRI WA HABARI STJOSO:
Uongozi wa St. Joseph’s College umewashukuru wanafunzi wote walioshiriki na kuchangia katika zoezi hili muhimu la kijamii. Ziara hii ni darasa la maisha ambalo linaendelea kujenga kizazi cha viongozi wenye utu, busara na huruma.
Comment hapa 👇
JibuFutaHakuna hela iliyokabidhiwa 😀
Futa🙏🙏
JibuFutaWow! Congratulations
JibuFuta