Machapisho

𝐖𝐀𝐒𝐈𝐏𝐎𝐊𝐔𝐓𝐀𝐅𝐔𝐓𝐀, 𝐉𝐈𝐓𝐀𝐅𝐔𝐓𝐄

Picha
Na, Thadeo Gelema Katika maisha ya sasa yenye ushindani mkubwa, watu wengi hujikuta wakihangaika kutafuta kukubalika na kuthaminiwa na wengine. Wengine hufikia hatua ya kujilazimisha kuwa sehemu ya makundi au mahusiano yasiyoendana na wao, wakiamini hapo ndipo watapata thamani yao. Hata hivyo, ukweli ni tofauti kabisa. Kuna msemo unaosema: “ Wasipokutafuta, jitafute.” Huu si msemo wa kubeza wengine, bali ni ujumbe mzito unaotukumbusha kuwa thamani ya mtu inaanza ndani yake mwenyewe. Kabla ya kutaka kukubalika na wengine, ni muhimu kwanza kujitambua—kujua wewe ni nani, una uwezo gani, na unataka kufika wapi. Watu wengi hupoteza muda mwingi wakijaribu kuwafurahisha wengine au kutafuta nafasi katika maisha ya watu wengine. Lakini mara nyingi jitihada hizo huishia kuwaumiza au kuwavunja moyo, hasa pale wanapokosa kuthaminiwa. Hii ni kwa sababu wanatafuta nje kitu ambacho kinapaswa kuanzia ndani. Kujitafuta kunamaanisha kujijenga—kiakili, kifikra, na hata kiuchum i. Ni mchakato wa kujifunza...

𝐊𝐈𝐒𝐀 𝐍𝐘𝐄𝐓𝐈: 𝐊𝐀𝐌𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀𝐏𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐑𝐄𝐉𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈

Picha
Na, Thadeo Gelema Leo Aprili 14, 2026 Kamati ya Maridhiano mkoani Shinyang a imelipongeza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa juhudi zake za kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao, hususan katika kipindi hiki ambacho kumeibuka uvumi unaosababisha taharuki miongoni mwa wananchi ukidai kuwa mtu akiguswa begani hupoteza sehemu zake za siri kwa wanaume. Picha: Viongozi wa Kamati ya Maridhiano mkoani Shinyanga wakiwa katika kikao cha majadiliano, wakijadili masuala ya kuimarisha amani, mshikamano na utulivu Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano,amani, mila na desturi mkoani humo, Shekhe Balilusa Khamis , akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, akiwa ameambatana na viongozi wengine wa dini mbalimbali, Mkuu wa Machifu pamoja na Kamanda wa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi. Amesema kuwa juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hofu kwa wananchi na kurejesha hali ya utulivu katika jamii. Picha: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mar...

𝐒𝐇𝐀𝐑𝐎𝐍 𝐀𝐀𝐏𝐈𝐒𝐇𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐒𝐓𝐉𝐎𝐒𝐎 2026/27, 𝐕𝐈𝐂𝐄𝐍𝐓 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐌𝐙𝐈𝐓𝐎

Picha
  Na Thadeo Gelema, Shinyanga Leo Aprili 13, 2026 Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, Sharon Callist Mathias,   ameapishwa rasmi kushika wadhifa huo, akiahidi kuanza kazi mara moja kwa kushughulikia changamoto zinazowakabili wanafunzi, ikiwemo suala la bima ya afya ambalo amelipa kipaumbele cha juu. Hafla ya kuapishwa iliyofanyika chuoni hapo imehudhuriwa na viongozi wa chuo, wanafunzi pamoja na wageni mbalimbali, huku ikitawaliwa na matumaini mapya ya uongozi. Akizungumza baada ya kula kiapo, Sharon alisema kuwa uongozi wake utaanza kwa kugusa mahitaji ya msingi ya wanafunzi. “ Kipaumbele changu cha kwanza ni kushughulikia changamoto ya bima ya afya kwa wanafunzi, pamoja na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya makatibu na vifaa vya uandishi wa habari ,” alisema Shaloni. Aidha , alisisitiza kuwa ataimarisha mahusiano kati ya wanafunzi, walimu, serikali ya chuo pamoja na taasisi binafsi ili kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kushirikiana. Kwa upande ...

𝐉𝐄, 𝐔𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐔? 𝐊𝐀𝐌𝐀 𝐇𝐔𝐍𝐀 – 𝐓𝐄𝐍𝐆𝐄𝐍𝐄𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐔!

Picha
  Na, Thadeo Gelema Katika maisha ya sasa, kuna ukweli mmoja ambao watu wengi huuchelewesha kuuelewa — maisha hayaendi peke yako . Wapo wanaoamini juhudi binafsi pekee zinatosha, lakini ukweli ni kwamba mafanikio mengi duniani yanabebwa na kitu kimoja kikubwa: watu (connections). Hebu jiulize maswali haya ya msingi: Siku ukipata tatizo kubwa, nani atasimama upande wako? Siku ukikosa hata pesa ya chakula, nani atakusaidia? Siku ukipata nafasi ya kazi au fursa, nani atakukumbuka? Kama majibu ya maswali haya ni hafifu — basi kuna kazi ya kufanya.   NGUVU YA KUWA NA WATU Maisha yana changamoto nyingi zisizotabirika. Leo uko vizuri, kesho hali inaweza kubadilika ghafla. Katika nyakati kama hizi: Rafiki anaweza kuwa msaada wa haraka kuliko ndugu Connection inaweza kufungua mlango ambao elimu peke yake haiwezi Mtandao wa watu unaweza kukuokoa pale sheria, pesa au nguvu hazitoshi Ndiyo maana inasemwa: “ Dunia siyo pesa, dunia ni watu.”   UKWELI MGUMU UNAOPASWA KUJUA Leo hii: Elim...

𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗢: 𝗦𝗛𝗔𝗥𝗢𝗡 𝗔𝗩𝗨𝗡𝗝𝗔 𝗨𝗞𝗨𝗧𝗔 𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢

Picha
  📅 10 Aprili 2026 Shinyanga – Hatimaye pazia limefungwa katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, huku Sharon Callist Mathias akiandika historia kwa kuibuka mshindi na kuwa Rais mpya wa wanafunzi. Uchaguzi huo uliokuwa umejaa presha, mvutano na matarajio makubwa, umegeuka kuwa gumzo kubwa chuoni hapo baada ya kuleta matokeo tofauti kabisa na uchaguzi wa awali.   MATOKEO RASMI YA MARUDIO Sharon (Shaloni) — kura 23 Vicent — kura 11 Moris Daudi — kura 8 Maduhu — kura 5 Sitta — kura 2  Jumla ya kura: 49  Hakuna kura iliyoharibika   ILIVYOKUWA MWANZO Katika uchaguzi wa kwanza, hali ilikuwa tofauti kabisa ambapo Maduhu aliongoza kwa kura 43, akifuatiwa na Sharon aliyepata kura 21. Hata hivyo, malalamiko juu ya mwenendo wa uchaguzi yalizua sintofahamu na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi.   MABADILIKO MAKUBWA Uchaguzi wa marudio umeonyesha mabadiliko ya wazi ya maamuzi ya wapiga kura, ambapo Shaloni ameweza kupindua upepo na kuibu...

𝗞𝗜𝗦𝗔 𝗡𝗬𝗘𝗧𝗜 𝗪𝗔𝗛𝗨𝗞𝗨𝗠𝗜𝗪𝗔 𝗝𝗘𝗟𝗔 𝗦𝗛𝗜𝗡𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔

Picha
Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamehukumiwa kifungo cha jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo zilizosababisha taharuki katika jamii. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Aprili 9, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi , aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Kisaka Elininhaki (22 ), mfanyabiashara, pamoja na Makoye James (20 ), dereva. Kwa mujibu wa Kamanda Magomi , watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kusambaza taarifa zisizo za kweli wakidai kuwepo kwa siri iliyopotea kimujiza baada ya kuguswa na benga, hali iliyozua hofu na taharuki kwa wananchi. Ameeleza kuwa baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama, wawili hao walipatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo. Katika hukumu iliyotolewa, Kisaka Elininhaki amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela , huku Makoye James akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela. Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakumbusha wananchi kuwa kusambaza taarifa za uo...

𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗪𝗔 𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢: 𝗝𝗘, 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗗𝗜𝗢 𝗙𝗨𝗥𝗦𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗞𝗜 𝗔𝗨?

Picha
  Na, Thadeo Gelema  📅 08 April 2026 | ⏰ Saa 15:20 Alasiri  Shinyanga – Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) limehitimishwa rasmi, lakini hadi sasa hali ya sintofahamu imeendelea kutawala baada ya matokeo kuchelewa kutangazwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo , zoezi la kupiga kura lilikamilika majira ya saa sita, huku kura zikihifadhiwa ndani ya chumba cha Dean of student , zikisubiri hatua zinazofuata katika mchakato wa kuhesabu na kutangaza matokeo. Hadi sasa , baadhi ya wagombea pamoja na wafuasi wao bado wapo eneo la tukio wakisubiri, huku wakitarajia uwepo wa Mkurugenzi wa chuo ili kuendelea na hatua inayofuata. Wakati huo huo, baadhi ya wanafunzi wameanza kuondoka kutokana na kuchelewa kwa mchakato huo. Hali hii imeendelea kuibua maswali miongoni mwa wanafunzi kuhusu uwazi na ufanisi wa usimamizi wa uchaguzi huo wa marudio, ambao tayari umebeba matarajio makubwa ya kurejesha imani ya wanafunzi. Kwa ujumla , Wakati mac...