PIGO KWA KANISA KATOLIKI: KARDINALI PENGO AFARIKI

Na, Thadeo Gelema
Kanisa Katoliki nchini Tanzania limeingia katika maombolezo kufuatia kifo cha Mhashamu Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 19, 2026 majira ya saa 4:00 akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu
Taarifa rasmi kutoka Jimbo Kuu la Dar es Salaam imethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa taratibu na ratiba za mazishi zitatolewa baadaye baada ya mipango kukamilika. Kardinali Pengo alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Kanisa Katoliki waliotoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani, maadili, amani na mshikamano wa kitaifa. Katika kipindi chote cha utumishi wake, alijulikana kwa sauti yake ya busara katika masuala ya kijamii, kiroho na kitaifa, jambo lililompa heshima kubwa ndani na nje ya nchi
Kwa ujumla, Kifo cha Kardinali Pengo ni pengo kubwa kwa Kanisa na Taifa kwa ujumla. Ataendelea kukumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka na huduma yake kwa Mungu na jamii. 
*Bwana ampe pumziko la milele.*


  



Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀