Breaking news
BREAKING NEWS: Spika Mstaafu Job Ndugai Afariki Dunia Jijini Dodoma
Mheshimiwa Job Yustino Ndugai enzi za uhai wake |
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Spika Mstaafu na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai.
Taarifa rasmi imetolewa leo tarehe 6 Agosti 2025 na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb), ambaye ameeleza kuwa Mhe. Ndugai amefariki dunia Jijini Dodoma.
"Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo Jijini Dodoma," amesema Mhe. Spika.
Aidha, Dkt. Tulia ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wananchi wa Kongwa, Wenyeviti wa Mungano, pamoja na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. "Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” ameongeza.
Bunge limeeleza kuwa linaendelea kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya marehemu katika kuratibu mipango ya mazishi. Taarifa zaidi zitatolewa kadri maandalizi yanavyoendelea.
Maoni
Chapisha Maoni