Machapisho

VIJANA SHINYANGA TUMIENI FURSA ZA KIUCHUMI KUJIKWAMUA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, amewataka vijana wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kuwa watazamaji wa masuala ya kiuchumi na badala yake wawe washiriki wakuu katika kuleta maendeleo ya mkoa na taifa. Akizungumza Februari 21, 2026 wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Vijana mkoani humo, Nanauka amesema Serikali imeweka mazingira rafiki kwa vijana kupitia mikopo, mafunzo ya ujuzi na matumizi ya teknolojia ili kuwawezesha kujiajiri na kukuza biashara. Amesisitiza kuwa vijana wana nafasi kubwa ya kuanzisha viwanda vidogo, kujenga mitandao ya biashara na kuongeza thamani ya rasilimali zilizopo. Aidha, amebainisha kuwa tayari mikataba zaidi ya saba imeingiwa kwa ajili ya kuwapeleka vijana kufanya kazi nje ya nchi, huku shilingi bilioni 200 zilizotolewa na Rais zikianza kutumika kuwawezesha vijana kiuchumi. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetolewa kupitia mikopo ya asilimia 10 mkoani Shinyanga, pamoja na ...

RADI YAUWA WATATU WAKIJIFICHA CHINI YA MTI MBEYA

Picha
Na Mwandishi wetu Mbeya   Watu watatu akiwemo mwanaume mmoja na wanawake wawili wakazi wa Kitongoji cha Goye, Kijiji cha Goye, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa wakiwa wamejificha chini ya mti wa asili. Kwa mujibu wa ndugu wa familia, waliotajwa kufariki dunia ni Wilson Sanga (27), Sikuzani Tumaini Sanga (39) na Lucia Joseph Mlumbe (49). Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa saba mchana, Februari 19, 2026, wakati watatu hao walipokuwa wakivuna mahindi shambani.  Mvua kubwa iliyoambatana na radi ilipoanza kunyesha, waliamua kujikinga chini ya mti wa asili, ndipo radi ilipowapiga na kusababisha vifo vyao papo hapo. Mwenyekiti wa Kitongoji alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji, ambaye aliarifu Jeshi la Polisi na kisha askari walifika eneo la tukio na kuuchukua miili ya marehemu na kuipeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Makandana, Tukuyu kwa ajili ya uchunguzi zaidi...

MSAKO WAANZA: POLISI ARUSHA MAUAJI YA MFANYABIASHARA WA MADINI

Picha
Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu wanaohusishwa na mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Abdillah Musa Mollel maarufu kama Banjo. Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa, Februari 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo, amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na linahitaji ushirikiano wa jamii ili kuwabaini wahusika. Kamanda Masejo ameeleza kuwa Februari 13, 2026 Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kupotea kwa mfanyabiashara huyo, ndipo msako na uchunguzi ulipoanza mara moja. Amedai kuwa wakati uchunguzi ukiendelea, Februari 19, 2026 walipokea taarifa za kuonekana kwa mwili wa marehemu katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ukiwa tayari umefariki. Marehemu Banjo, ambaye alikuwa akiishi katika eneo la Sanawari jijini Arusha, inadaiwa alionekana kwa mara ya mwisho hadharani alipokuwa akifanya mazoezi ya mwili katika...

PIGO KWA KANISA KATOLIKI: KARDINALI PENGO AFARIKI

Picha
  Na, Thadeo Gelema Kanisa Katoliki nchini Tanzania limeingia katika maombolezo kufuatia kifo cha Mhashamu Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 19, 2026 majira ya saa 4:00 akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu Taarifa rasmi kutoka Jimbo Kuu la Dar es Salaam imethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa taratibu na ratiba za mazishi zitatolewa baadaye baada ya mipango kukamilika. Kardinali Pengo alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Kanisa Katoliki waliotoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani, maadili, amani na mshikamano wa kitaifa. Katika kipindi chote cha utumishi wake, alijulikana kwa sauti yake ya busara katika masuala ya kijamii, kiroho na kitaifa, jambo lililompa heshima kubwa ndani na nje ya nchi Kwa ujumla, Kifo cha Kardinali Pengo ni pengo kubwa kwa Kanisa na Taifa kwa ujumla. Ataendelea kukumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka ...

CHUKUENI TAHADHARI MNAPOKIMBIA MCHAKAMCHAKA BARABARANI

Picha
picha: Askari Polisi Koplo Zuhura Mlungwana akiwapa maelekezo ya usalama. Hii ni Thadeo Media  Leo Jumatano ya Februari 18, 2026 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyashimbi iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani Kwa kuchukua tahadhari pindi wawapo katika mazoezi ya mchakachaka barabarani. Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Kahama Koplo Zuhura Mlungwana amewaelimisha wanafunzi hao kujipanga upande wa kushoto wa barabara ikiwa ndio upande sahihi wa kukimbilia wakiwa katika mazoezi yao pamoja na kuwapanga washika vibendera mbele ya kundi na nyuma ili waweze kuongoza kundi hilo barabarani  Koplo Zuhura amewasisitiza kujipanga mistari mitatu hadi minne wakati wa mazoezi ili kupunguza msongamano barabarani na kuepuka ajali pindi watakapo kanyagana na kuanguka. Picha: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyashimbi wakiwa kwenye mazoezi ya mchakachaka barabarani, wakiwa wamepangwa vizuri huku polisi akiwapa ma...

KAULI ZA WATU WASIO NA MALENGO KATIKA KAZI / BIASHARA

Picha
Imeandaliwa na: Up-line: Thadeo Gelema, Thadeo Media Katika dunia ya kazi na biashara, mafanikio huanza na mtazamo wa mtu. Watu wengi hushindwa si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu ya kauli wanazojenga akilini mwao. Kauli hizi hugeuka kuwa vizuizi vinavyokwamisha maendeleo yao kila siku. Kauli Zinazowarudisha Nyuma Wengi “ Sina mtaji” Mtaji si fedha pekee. Ujuzi, muda, nguvu na mtandao wa watu ni rasilimali tosha kuanza hatua ndogo. Wengi waliofanikiwa walianza na walichokuwa nacho. “ Nitaanza lazima kesho” Kesho isiyofika ndiyo adui wa mafanikio. Kila mafanikio huanza na hatua ya leo, hata kama ni ndogo. “ Sina mawasiliano” Mahusiano hujengwa. Kushiriki kwenye matukio, kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kujitambulisha kwa watu hufungua milango ya fursa. “ Mimi ni wa hivi hivi tu” Hii ni kauli ya kujidharau. Ukuaji wa mtu hutegemea namna anavyojiona. “ Ndugu zangu wamenitenga” Mafanikio ni jukumu binafsi. Wengi waliofanikiwa walianza bila msaada wa karibu. “ Sina bahati” Baha...

DONDOO KUTOKA KURASA MAGAZETI YA 18, FEBRUARY, 2026

Picha