Machapisho

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

Picha
  Na mwandishi wetu,Njombe Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji. "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga. Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo aska...

DONDOO KUBWA KUTOKA KURASA ZA MAGAZETI YA JANUARY 29, 2026

Picha
Hii ni Thadeo Media  Magazeti ya leo                                    

SH. 200 BILIONI KWA VIJANA NA INTERNET NAFUU KUCHOCHEA

Picha
 Hii ni Thadeo Media   Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limegeuka kuwa jukwaa la matumaini kwa vijana nchini kufuatia wabunge na viongozi wa serikali kuainisha fursa kemkem zilizowekwa ili kukuza uchumi wa kizazi hicho.  Akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wakati wa ufunguzi wa Bunge la kumi na tatu, Mbunge wa Bunda Mjini, Mheshimiwa Ester Bulaya, amewahimiza vijana nchini kuchangamkia fursa zinazoletwa na serikali ya awamu ya sita akibainisha kuwa utekelezaji wa ahadi kubwa za Rais kuelekea kundi hilo tayari umeanza kwa vitendo. Mheshimiwa Bulaya amefafanua kuwa miongoni mwa mambo makubwa yaliyofanyika ni uamuzi wa Rais kutoa kipaumbele kwa vijana katika wizara zote pamoja na kutenga kiasi cha shilingi bilioni mia mbili kwa ajili ya vijana wajasiriamali nchini kote.  Aidha, amebainisha kuwa serikali imejikita katika kuwajengea vijana mazingira bora ya kufanya biashara na kuanzisha kampasi za vyuo katika maeneo mbalimbali ili kuwaandaa kitaaluma na kiufundi ...

MWENYEKITI UMIKIDO AKUTANA NA WAZIRI KATAMBI KUJADILI MAADILI YA HABARI MTANDAONI

Picha
 Hii ni Thadeo Media   Dodoma . Mwenyekiti wa Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, leo Januari 28, 2026 Majata alimweleza Waziri Katambi juu ya malengo ya UMIKIDO katika kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali. Waziri Katambi amepongeza hatua ya umoja huo kujitambulisha, na ameuhimiza UMIKIDO kufika ofisini kwake ili kufanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimaadili, matumizi salama ya mitandao, pamoja na namna vyombo vya habari mtandaoni vinavyoweza kushirikiana na serikali katika kulinda usalama na maslahi ya Taifa

POLISI ARUSHA WAMKAMATA MWANACHAMA WA CHADEMA KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA TUNDU LISSU

Picha
  Na mwandishi wetu, Arusha Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu". Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa. "Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masejo....

HUU NI WAKATI WA VIJANA KUACHA KUONA SEKTA YA MADINI KAMA YA WENYE MITAJI MIKUBWA PEKEE

Picha
Hii ni Thadeo Media  Sekta ya madini nchini imepiga hatua kubwa ya kihistoria baada ya Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya mataifa yenye akiba kubwa ya madini barani Afrika, hatua inayotajwa kuwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa, uzalishaji wa ajira na kuongezeka kwa fursa za kiubunifu kwa vijana. Akizungumza jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya siku 100 za kwanza za kipindi cha pili cha uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema Tanzania imefanikiwa kununua tani 17 za dhahabu ndani ya siku 100 pekee. Hatua hiyo imeimarisha akiba ya taifa na kuongeza mchango wa sekta ya madini kutoka asilimia 10.1 hadi asilimia 11.2 ya Pato la Taifa. Ameeleza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na sera thabiti za serikali zinazovutia uwekezaji wa ndani na nje, hususan katika ujenzi wa viwanda vya kusafisha na kuyeyusha madini ndani ya nchi. Hatua ya kuachana na utaratibu wa kusafirisha madini ghafi imefungua milang...

DONDOO KUBWA KUTOKA KURASA ZA MAGAZETI YA JANUARY 28, 2026

Picha
Hii ni Thadeo Media  Magazeti