Machapisho

Habari

Picha
  UCHAGUZI MDOGO 2025: Wananchi Fuoni, Siha na Kata 5 Wajitokeza kwa Wingi Kupiga Kura Mkazi wa Shehia ya Migombani katika jimbo la Fuoni akipiga kura leo kumchagua Mbunge wa jimbo hilo.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taiofa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele akiwa na mkazi wa Shehia ya Fuoni aliyekua akihakiki jina lake kabla ya kuingia kupiga kura leo.  Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akizungumza mmoja wa wasimamizi wa viuo vya kupigia Kura katika jimbo la Fuoni Mjini Zanzibar leo.  Mkazi wa Shehia ya Migombani katika jimbo la Fuoni akipiga kura leo kumchagua Mbunge wa jimbo hilo katika kituop cha Skuli ya Raudha B.  Mwenyekiti wa Tume na Mjumbe wa Tume hiyo wakizungumza na Mawakala katika moja ya vituo vya kupigia Kura.  Wananchi wa Jimbo la Fuoni na Siha pamoja na Kata tano za Tanzania bara wamejitokeza kwawingi kupiga kura leo Desemba 30,2025 katika Uchaguzi mdogo uliofanyika katika majimbo yao. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya...

Habari

Picha
Kesi ya Jengo la Ghorofa Kariakoo: Wawili Waachiwa Huru, Hatima ya WashtakiwaWanne Yabaki Kitendawili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washtakiwa wawili kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa, eneo la Kariakoo. Wawili hao ambao ni Zenabu Silam (61) na Ashour Awadhi Ashour (38) wameachiwa huru leo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kusema hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao. Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Olembelle kumueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ya kwamba DPP amewasilisha hati ya kutoendelea na kesi dhidi ya washtakiwa hao wawili. Washtakiwa wanne waliobaki katika kesi hiyo ni Leondela Mdete (49), Soster Nziku (55), Aloyce Sangawe (59) na Stephen Nziku (28) wote ni wakazi wa Dar es Salaam. Washtakiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo, Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Congo eneo la Kariakoo ambapo isivyo halali walishindwa kutimiz...

Habari

Picha
 ‘ Sijawahi Kuona Kitu Kama Hiki’ — Jinsi Nyuki Walivyozuia Jaribio la Wizi Katika Duka Tunduma. Mimi ni Andulike, na ninamiliki duka dogo la jumla katika eneo la Mpemba, Tunduma. Nimekuwa nikiendesha kwa miaka kumi, nikiuza kila kitu kuanzia vitu vya nyumbani hadi vitafunio, na hata mimea michache niliyoilima mwenyewe kutoka kwenye bustani yangu. Sio mahali pazuri, lakini imekuwa fahari yangu kila wakati. Sikuwahi kufikiria kwamba asubuhi moja ya kawaida ya Jumatatu ingegeuka kuwa moja ya siku zisizosahaulika zaidi maishani mwangu. Siku ilianza kama nyingine yoyote. Jua lilikuwa linachomoza tu, likitoa mwanga laini wa rangi ya chungwa mitaani. Wateja waliingia kwa upole, watoto walipita mbio njiani kuelekea shuleni, na waendesha pikipiki walipiga honi kupitia barabara zilizojaa watu. Nilikuwa nimefungua duka langu, nikipanga vitu kwenye rafu, nilipoona wanaume wawili wakizurura karibu na mlango kwa mashaka. Walikuwa wamevaa hoodies nyeusi na waliendelea kutazama mabegani mwao kwa ...

Magazeti

Picha
Dondoo Kubwa Kutoka Kurasa za Magazeti ya Desemba, 30, 2025                          

Habari

Picha
 Dkt. Mwinyi Aongoza Baraza la Mapinduzi na Kuapisha Mkuu wa Mkoa Na Thadeo Media  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao cha Kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) cha Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Disemba 2025, Ikulu, Zanzibar. Kikao hicho cha BLM pia kimeambatana na uapisho, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya, aliyemteua hivi karibuni. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mgeni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba. Kikao hiki kinaashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali ya Awamu ya Nane katika Kipindi cha Pili, kikionesha dhamira ya kuimarisha utawala bora na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.

Magazeti

Picha
Dondoo Kubwa Kutoka Kurasa za Magazeti ya Desemba, 29, 2025