EPUKENI KUFANYA BIASHARA SEHEMU HATARISHI

 Hii ni Thadeo Media 


Wafanyabiashara wanaouza mazao ya chakula na mbogamboga pembezoni mwa Daraja la Kidalu katika Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari makini wanapoendelea na shughuli zao, kutokana na hatari kubwa ya ajali inayoweza kutokea katika eneo hilo.

​Wito huo umetolewa na Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, wakati akizungumza na wafanyabiashara hao ambapo amesema kuwa kusimama karibu na eneo la daraja ni hatarishi kwa sababu magari na vyombo vya moto vinaweza kukosa uelekeo jambo ambalo linaweza kusababisha ajali kwa wafanyabiashara, wateja na watumiaji wengine wa barabara.

​Aidha, aliwasisitiza wanapofanya biashara pembezoni mwa barabara kuhakikisha wanaweka alama au vitu vinavyoonekana vizuri vya onyo ili kuwatangazia madereva kuhusu uwepo wao, jambo litakalosaidia kupunguza hatari za ajali.

Kwa ujumla, Jeshi la Polisi Shinyanga linasisitiza kuwa usalama wa wafanyabiashara na wateja katika eneo la Daraja la Kidalu unategemea umakini wao na matumizi ya alama za onyo ili kuepusha ajali zinazoweza kusababishwa na magari kupoteza uelekeo.

Picha:Sajenti David Ndimila wa Usalama Barabarani Shinyanga akitoa elimu ya tahadhari kwa wafanyabiashara pembezoni mwa Daraja la Kidalu kutokana na hatari ya ajali.





Maoni