Vilabu vinne vya Tanzania Kesho Kuanza Safari ya Kimataifa CAF Na Thadeo Gelema Septemba 18, 2025 Vilabu vinne vikubwa vya Tanzania – Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Singida Black Stars – vipo tayari kwa mapambano ya kimataifa katika michuano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup wikiendi hii, ambapo mchezo wa kwanza utaanza kesho Ijumaa, Septemba 19, 2025 . Yanga SC vs Wiliete SC (Angola) Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wataanza safari yao kwa kuvaana na Wiliete SC ya Angola kesho Ijumaa, Septemba 19, saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Estádio 11 de Novembro huko Benguela. Marudiano yatapigwa Dar es Salaam, Septemba 26, 2025. Azam FC vs El Merrikh SC (Sudan) Katika michuano ya CAF Confederation Cup, Azam FC nao wataanza kesho Ijumaa, Septemba 19, saa 12:00 jioni , dhidi ya El Merrikh SC ya Sudan kwenye Uwanja wa Juba National Stadium , Sudan Kusini. Marudiano yatafanyika Dar es Salaam, Septemba 26, 2025. Singida Black Stars vs Rayon Sports (Rwand...