𝐇𝐀𝐖𝐀 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐀 𝐌𝐌𝐄𝐘𝐀𝐊𝐀𝐕𝐘𝐀𝐆𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐙𝐈 𝐒𝐓𝐉𝐎𝐒𝐎 2026/2027! 🔥
Na, Thadeo Media Leo Machi 26, 2026 Shinyanga – Mjadala umeendelea kupamba moto kufuatia matokeo ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, huku baadhi ya wagombea waliopoteza wakionekana kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi huo. Miongoni mwa majina yanayotajwa sana ni pamoja na Mh. Vicent Chacha, Mwl. Moris Daudi, Sitta Matias pamoja na Sharon , ambao kwa nyakati tofauti wameonekana kuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa wanafunzi kabla ya uchaguzi huo. Wafuasi wa wagombea hao walianza kutoa kauli kali, wakisisitiza kuwa hawako tayari “ kuludi vyuma”, wakimaanisha kuwa bado wanashikilia misimamo yao na hawajaridhika kirahisi na matokeo yaliyotangazwa. Vicent Chacha, anayejulikana kwa msimamo wake thabiti na uzoefu wa uongozi, anaendelea kutajwa kama kiongozi mwenye ushawishi mkubwa hata baada ya matokeo. Kwa upande wake, Mwl. Moris Daudi , aliyekuwa na wafuasi wengi kutokana na ukaribu wake na wanafunzi na shughuli za kijamii, bado anaonekana ku...